Witsel, Trippier kukutana Newcastle

0
93

MUNICH, Ujerumani

NEWCASTLE United inampigia hesabu kiungo wa Borussia Dortmund raia wa Ubelgiji, Axel Witsel, sambamba na beki wa pembeni wa Atletico Madrid, Kieran Trippier.

Mkataba wa Witsel utafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu, ambapo Newcastle watamnasa bure endapo watasubiri hadi kufikia kipindi hicho.

Mbali ya wawili hao, pia klabu hiyo inampigia hesabu ndefu mshambuliaji wa Liverpool, Divock Origi.

Hata hivyo, huenda ikawa ngumu kwa Origi kwani Liverpool wameonesha kutokuwa tayari kumfungulia mlango wa kutokea.

Source: mtanzania.co.tz