Wabunifu, wanamitindo chipukizi kuchuana jukwaa moja

0
64

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MAONYESHO ya mavazi kwa wabunifu na wanamitindo wachanga yanayojulikana kama Start Tailoring Business (STB) yanatarajia kufanyika Novemba 27,2021 katika  Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtanzania Digital jijini Dar es Salaam,  Mratibu wa maonyesho hayo, Augustar Masaki, amesema jumla ya wanamitindo 30 na wabunifu 15 watashiriki.

“Nimekuwa na darasa kwa vijana wanaopenda kuwa wabunifu. Mwaka huu tumepata wenye ulemavu ambao tutashiriki nao katika jukwaa hilo la mavazi,” amesema Masaki.

Amesema mavazi yatakayoonyeshwa yametengenezwa na wahitimu ambao pia watatunukiwa vyeti na zawadi kwa watakaofanya vizuri zaidi.

Source: mtanzania.co.tz