Villarreal yampa ‘CR7’ bao la 800

0
71

VILLARREAL, Hispania

STAA wa Manchester United, Cristiano Ronaldo, jana alifikisha mabao 800 katika maisha yake ya soka baada ya kufunga moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji wao, Villarreal.

Katika mtanange huo wa hatua ya makundi, Ronaldo aliitanguliza Man United katika dakika ya 78, kabla ya Jadon Sancho kuweka jingine dakika 12 baadaye.

Huku hilo likiwa ni la 800 tangu aanze kucheza soka la kulipwa, pia lilikuwa la 140 katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.

‘CR7’, licha ya umri wake wa miaka 36, amecheka na nyavu katika kila mchezo wa msimu huu wa mashindano hayo, akiwa ameshafunga mabao sita.

Source: mtanzania.co.tz