Gerrard: Traore hauzwi jamani

0
120

LONDON, England

KATIKA kukiimarisha kikosi chake, kocha mpya wa Aston Villa, Steven Gerrard, ameweka wazi kuwa staa wake raia wa Burkina Faso, Bertrand Traore, hauzwi.

Kwa muda mrefu Traore amekuwa akizitoa udenda klabu kadhaa kubwa barani Ulaya, ikiwamo Liverpool.

Wakati huo huo, Gerrard aliyejiunga na Villa hivi karibuni akitokea Rangers, anataka kuliimarisha eneo la ulinzi kwa kuongeza beki wa kati wakati wa usajili wa Januari, mwakani.

Katika hilo, tayari ameshawaambia mabosi wa timu hiyo kuhakikisha wanainasa saini ya mlinzi wa Kihispania anayetikisa La Liga akiwa na Villarreal, Pau Torres.

Source: mtanzania.co.tz