Courtois apotezea FIFA kumtosa

0
97

MADRID, Hispania

MLINDA mlango wa Real Madrid, Thibaut Courtois, amesema haimuumizi kichwa kutokuwamo kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka huu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Makipa waliotajwa kuiwania tuzo hiyo ni Alisson Becker, Gianluigi Donnarumma, Edouard Mendy, Manuel Neuer na Kasper Schmeichel.

Alichokisema kipa huyo tegemeo kwa Madrid na timu ya taifa ya Ubelgiji ni kwamba ameachwa kwenye tuzo hiyo kwa kuwa amekuwa akiikosoa mara kadhaa.

Baada ya majina kuwekwa hadharani, zoezi la kupiga kura lilianza Jumatatu ya wiki hii, likitarajiwa kufungwa Desemba 10, mwaka huu.

Source: mtanzania.co.tz