Alcantara: Barca? Bado nipo sana Liverpool

0
70

MERSEYSIDE, England

LICHA ya kuhusishwa na mpango wa kurejea Barcelona, kiungo wa Kihispania, Thiago Alcantara, amesema akili yake iko Liverpool tu.

Awali, zilikuwapo taarifa zinazodai kuwa lejendari aliyekabidhiwa mikoba ya kuinoa Barca, Xavi, anataka kuona kiungo huyo anarejea Nou Camp.

Hata hivyo, Alcantara amesema anataka kushinda mataji mengi akiwa Anfield na kuongeza kuwa anaiona Liver ya sasa ikiendana na Barca iliyokuwa ikinolewa na Pep Guardiola.

Kauli yake hiyo inaendana na alichokisema staa mwenzake wa zamani wa Barca, Lionel Messi, aliyeitaja Liver kuwa ndiyo timu tishio zaidi msimu huu wa Ligi ya Mabingwa.

Source: mtanzania.co.tz